Na. Paul Kasembo - SHY RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kurekebisha kasoro zote zilizojitokeza kwenye Mnio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ili kama Mkoa uweze kupata alama bora, nzuri zenye kuwezesha kupata ushindi.
Haya ameyasemamleo tarehe 8 Aprili, 2024 katika kikao cha kwanza cha Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Lewis Kalinjuna Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wakionhozwa na RAS Shinyanga Prof. Siza Tumbo na Wakuu wa Usalama Mkoa huku akisisitiza kila mmoja kutimiza wajibu wake.
"Nizitake Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kwenda kurekebisha kasoro zote zilizojitokezamwaka 2023 katika Mbio za Mwenge wa Uhuru, ili mwaka huu wa 2024 tupate alamanzuri zitakazotupatia ushindi," amesema Mhe. Macha.
Akimkaribisha katika kikao kazi hiki, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amesema kuwa, pamoja na mambo mengine lakini Mkoa wa shinyanga unatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 10 Agosti, 2024 kutokea Mkoa wa Simiyu na kukabidhi Mkoa wa Tabora tarehe 16 Agosti, 2024.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama alisisitiza na kuweka mkazo zaidi katika Miradi ya uwezeshwaji vijana kiuchumi na umuhimu wa kutumia wajasiriamali wa ndani ya Halmashauri na Wilaya zetu ili kuongezaia mzunguko wa redha katika eneo husika.
Kando na maelekezo haya, RC Macha ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa mshindj namba 11 Kitaifa kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ambapo amesema kuwa ni hatua nzuri sana kitaifa huku akizitaka Halmashauri zote kwenda kujiandaa vema na ujio wa Mwenge ifika Agosti, 2024.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa