Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita leo septemba 17,2025 amepokea vikombe viwili kutoka kwa Timu ya RS Shinyanga Sport Club kufuatia ushindi walioupata katika mashindano ya 39 ya Shirikisho la Michezo la Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Tawala za Mikoa (SHIMIWI), yaliyofanyika Jijini Mwanza kuanzia Septemba 1 hadi 16, 2025.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe hivyo kwa Mkuu wa Mkoa, Makamu Mwenyekiti wa RS Shinyanga Sport Club, Bw. William Masala, alieleza kuwa timu hiyo iliwakilishwa na washiriki 15 waliogawanywa kwenye michezo minane, ambapo walifanikiwa kufanya vizuri hasa katika mchezo wa karata na mbio za kupokezana vijiti.
Katika mashindano hayo, Timu ya Karata ya wanaume iliibuka Mabingwa wa Kitaifa, huku timu ya wanawake ikiibuka na nafasi ya tatu, na hivyo kuiwezesha RS Shinyanga Sport Club kurejea na vikombe viwili vya heshima.

Mhe. Mboni Mhita ameipongeza timu hiyo kwa kushiriki mashindano hayo kwa nidhamu, bidii na uzalendo, na kuwataka watumishi wa umma kuendeleza moyo huo wa ushirikiano na michezo kama njia ya kuimarisha afya na mshikamano mahala pa kazi.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni, aliwapongeza wanamichezo hao kwa kuiwakilisha vyema Shinyanga na kuliletea heshima kubwa Mkoa kwa kurudi na ushindi.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa