Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini sana kazi zote zinazofanywa na Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya Kiserikali likiwemo la World Vision Kanda ya Ziwa.
RC Macha ameyasema haya tarehe 29 Aprili, 2024 katika mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa World Vision Kanda ya Ziwa ukiongozwa na Meneja wa Kanda Bi. Jacqueline Kaihura ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine amewaahidi ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote huku akiwapongeza sana kwa namna wanavyotekeleza miradi yao ambayo inagusa maisha ya wananchi wa Shinyanga na maeneo mengine nchini.
"Napenda kuwaambia kwamba, Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua, inathamini kazi zote mnazozifanya World Vision Kanda ya Ziwa na jwa muktadha huu Serikali itaendelea kufanya kazi nanyi wakati wote, hongereni sana na karibuni tena Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga," amesema RC Macha.
Uongozi wa World Vision Kanda ya Ziwa wamefika Ofisini kwa RC Macha kwa lengo kujitakbulisha kwake na kueleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika Kanda hii ya Ziwa ambayo inajumuisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Tabora.
Kwa Mkoa wa Shinyanga WVT wanatekeleza miradi katika Wilaya ya Kishapu, Kahama na Shinyanga DC ambapo kuna miradi ya muda mfupi ambao ni GROW na NOURISH inayojumuisha afya ya mama na mtoto kuinua kipato cha familia, lishe na kilimo.
Huku miradi ya muda mrefu ikitajwa kuwa ni Kilago Area Program, Lagana Area Program na Mwakipoya Area Program.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa