Na Shinyanga RS.
Serikali imesema inatambua na kuheshimu mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika muktadha wa kuhabarisha umma na kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 18 Mei, 2023 na Mhe. Johari Samizi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakati akiongea na waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari alipomuwakilisha Mhe. Christina Mndeme ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club) katila Ukumbi wa Mikutamo uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano wa Serikali, lakini pia Mhe. Johari amekuwambusha juu ya umuhimu wa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari yenye weledi, tija na zenye kuelimisha jamii ili kuiheshimisha taaluma ya habari pamoja Taasisi zao wanazozifanyia kazi.
"Niwahakikishie kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana nanyi wakati wote kwakuwa inatambua na kuheshimu mchango wenu kwa umma na Taifa kwa ujumla, lakini pia niwatake mzingatie maadili ya taaluma zenu wakati wote mnapkuwa mnatekeleza majukumu yenu, nasi kwa upande wetu kama Serikali tupo tayari kupokea maoni yenu na hizi changamoto mlizowasilisha tumezichukua", alisema Mhe. Johari
Akitoa salamu kwa niaba ya Shinyanga Press Club Ndg. Greyson Kakuru pamoja na mambo mengine aliainisha baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi zao ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa Serikaki kuwa na urasimu wa kuwanyima taarifa za shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika, kupewa vitisho pindi wanapofichua miradi ambayo iko chini ya viwango na wanapofuatilia masuala ya kijamii ikiwamo yanayohusu ukatili wa kijinsia ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi Fransic Mihayo aliwaambia waandishi wa habari na wadau kuwa, ni vema kwa yeyote anayetaka kufanya kazi ya habari akasomea taaluma hiyo kikamilifu ili aendane na matakwa ya Sheria ya habari ya mwaka 2016, huku akiwataka wale wote wanaoendesha shughuli za kuhabarisha wananchi kupitia Online TV au Blogs kuzisajili na kupata leseni zitakazo waruhusu kufanya kazi hizo bila usumbufu.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani hufanyika kila mwaka Mei 3 kwa ajili ya kufanya tathimini ya mchango wa vyomno vya habari ambapo Mkoa wa Shinyanga umeadhimisha tarehe 18 Mei, 2023 kwa kuzingatia ratiba kutoka Umoja wa Klabu za Habari Tanzania (UTPC) ambao unaagiza kila Klabu kupanga tarehe ya maadhimisho ndani ya mwezi Mei.
Picha ikionesha baadhi ya wanahabari na washiriki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mhe. Johari Samizi wakati wa maadhimisho
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa