Na. Shinyanga RS
MKUU wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020/2025 kwa vitendo na kwa weledi mkubwa ili kuwaletea maendeleo wananchi huku akisisitiza kuwa na ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Haya yamesemwa leo tarehe 20 Februari, 2024 wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga katika Halmashauri ya Ushetu ambapo jumla ya miradi ya maendeleo mitatu ikiwemo Shule ya Sekondari Dakama, Shule ya Msingi Ukune na Hospitali ya Halmashauri ya Ushetu ambapo kabla ya kukaguliwa mradi wa mwisho Kamati pia ilifanya Mkutano wa hadhara katika kijiji cha cha Ukune ambapo imepokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
"Ndugu Mabala Mlolwa Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, wajumbe wa kamati na wananchi wote, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme napenda kusema kuwa sisi Serikali tatuendelea kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo, kwa weledi mkubwa sana na tunatekeleza ahadi ya CCM ya kuwaletea maendeleo yenye tija kupitia sekta mbalimbali kama inavyojionesha kwenye miradi hii ya kimkakati", amesema Mhe. Mboni.
Pamoja na pongezi kwa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo na Serikali ya Mkoa kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa wananchi, lakini pia Mwenyekiti wa Kamati Ndg. Mabala Mlolwa ameishauri Serikali kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili kuona umuhimu wa kuchangia chakula kwa wanafunzi mashuleni ili waweze kupata chakula mchana au uji asubuhi jambo ambalo litatoa hamasa ya kusoma, kupunguza kabisa utoro na kuimarisha usikivu kwa wanafunzi darasani.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga inaendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kuona jinsi gani Ilani ya CCM 2020 / 2025 inavyotekelezwa katika Mkoa ambapo leo ni zamu ya Halmashauri ya Msalala, na kesho tarehe 21 Februari ni zamu ya Manispaa ya Kahama.
HABARI PICHA
Picha hapo juu ni muonekano wa baadhi ya majengo na vifaa tiba katika Hospitali ya Halmashauri ya Ushetu - Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa