Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa kata za Kagongwa na Isaka kuanza kutumia maji kutoka mradi mkubwa unaotekelezwa na Serikali kuu kwa gharama ya sh. Bil 24.7.
Akizungumza na wananchi katika kijiji cha Isagehe mapema leo baada ya kukagua mradi huo, amewataka kuwapuuza viongozi na watu wanaopotosha kwa kueneza uzushi kuwa hawatapa maji licha ya mradi kuelekea kukamilika.
Naye Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema, Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanaondokana na tatizo la maji.
Mradi huo wenye matenki ya ujazo wa lita milioni 1.6, umekamilika kwa 60% na utaanza kufanya kazi mwezi Juni mwaka huu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa