Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MGANGA Mkuu Mkoa wa Shinyanga Daktari. Yudas Ndungile kwa niaba ya Serikali ya Mkoa amepokea Madawa kwa ajili ya kukinga magonjwa ya kuhara na kipindupindu kutoka Shirika la World Vision Tanzania vyenye gharama ta Tzs. Milion 5 Lengo ni kuwakinga wananchi na magonjwa ya kuharisha na kipindupindu mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa dhati baina ya Serikali na Mashirika Binafsi katika utoaji wa huduma za afya.
Ameyasema haya leo tarehe 12 Novemba, 2024 wakati akikabidhiwa Madawa kwa ajili ya kukinga magonjwa ya kuhara na kipindipindu Mkoa wa Shinyanga ambavyo ni drip za maji, vidonge vya kutakasa maji nk. katika utekelezaji wa awamu ya kwanza (1) wa kuzuia magonjwa ya mlipuko.
“Nawapongeza sana Shirika la World Vision kwa ushirikiano mzuri ambao mmekuwa mkiuonesha kwa Serikali kupitia sekta ya afya kwani madawa haya yanakwenda kutusaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindukipindu na maradhi mengine katika msimu huu wa mvua”, amesema Daktari. Yudas.
Akikabidhi vifaa tiba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Vision Tanzania, Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa Bi. Shukrani Dickson amesema wameguswa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliotokea Wilaya ya Kishapu hivyo wameitikia wito kwa kutoa dawa hizi huku akiwaasa wananchi kuzingatia usafi na utunzaji wa mazingira katika makazi yao ili kuzuia ugonjwa huu kusambaza zaidi.
Shirika la Wold Vision Tanzania linashirikiana na Serikali na wadau wengine katika ngazi zote kuboresha mfumo wa huduma za afya kwa kutoa vifaa kinga na tiba ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu hasa Wilaya ya Kishapu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa