MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amesema kuwa, kufuatia uwepo wa Ugonjwa wa Kuhara na Kutapika, Serikali ya Mkoa imejidhatiti vema kuondoa kabisa huku akiwataka wananchi kufuata na kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalam wa afya.
Haya yamesemwa na RC Mndeme alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya uwepo wa ugonjwa huu mkutano ambao umefanyika leo tarehe 9 Jan, 2024 ofisini kwake.
"Serikali ya mkoa tumejidhatiti vema kuondoa kabisa ugonjwa huu wa kuhara na kutapika, lakini pia nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi kufuata na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya ili kujinga na kudhibiti hali hii", amesema RC Mndeme.
Tarehe 28 Desemba, 2024 katika kata ya Kagongwa iliyopo Manispaa ya Kahama hapa mkoa wa shinyanga kulitokea vifo vya watu 5 ambavyo vilisababishwa na ugonjwa wa kuhara na kutapika.
Aidha, RC Mndeme amesema baada ya hapo serikali iliunda timu ndogo ya kuratibu na kufuatilia ugonjwa huo, ambapo baadae ilibaini uwepo wa wagonjwa 18 wa kipindipindu 15 kutoka Manispaa ya Kahama, wagonjwa 2 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na 1 kutoka Manispaa ya Shinyanga.
Kando na jitihada hizo, pia serikali imetenga Kambi tatu maalum za kufanya matibabu ya ugonjwa huu ambazo ni Kituo cha afya Ihapa kilichopo Manispaa ya Shinyanga, Kituo cha afya Kagongwa Manispaa ya Kahama, Kituo cha afya Kishapu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa