Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ameahidi kuwasaidia Tzs. Milioni 22 kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Kikundi cha Wanawake Lumolumo kilichopo Kijiji cha Namba Moja, Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala Mkoa wa Shinyanga.
Ahadi hiyo imetolewa wakati wa ziara ya Mhe. Mboni aliyemuwakilisha Mhe. Christina Mndeme Mkuu wa MKoa wa Shinyanga na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwamo UN- WOMEN, KOICA na TAHA ambapo alitembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ilkiwamo shamba, ushonaji upishi nk.
“Ombi lenu nimelipokea, na kwa bahati nzuri leo tupo wote hapa na Mkurugenzi wa Msalala, sasa nimuombe rasmi hapa hapa alichukue ombi lenu la Milioni 22 na aende akaliweke kwenye mpango wa mikopo isiyokwa na riba itolewayo na Halmashauri ili mwaka wa fedha ujao muweze kupewa na mfungue hilo duka lenu kama mradi wa kikundi na mfikie malengo yenu kama mlivyokusudia, hili limekwisha chapeni kazi,” alisema Mhe. Mboni.
Awali akisoma taarifa Mwenyekiti wa Kikundi cha Lumolumo alisema kwamba pamoja na mafanikio kiasi waliyoyapata, lakini waliomba wadau kutoka TAHA, UN-WOMEN na Halmashauri kuendelea kuwashika mkono kwa kuwazesha kuongeza mtaji ili waweze kufungua duka litakalokuwa na thamani ya Milioni 27 ambapo wao wanayo Milioni 5 zilizopo Benki.
Kufunguliwa kwa duka hilo kutapelekea kusogeza huduma karibu zaidi na wakulima wa Halmashauri ya Msalala na Kahama ambapo wataweza kupata mbegu na pembejeo na kwamba wanatarajia kuwa Wakala mkubwa na muhimu Zaidi kwa Mkoa wa Shinyanga.
Kikundi cha Lumolumo kilianzishwa rasmi Septemba, 2019 kikiwa na wananchama 12 wote wanawake, ambapo sehemu ya mafanikio ni pamoja na kuchimba kisima cha maji chenye urefu wa futi 100 chenye thamani ya Milioni 32, kutengeneza miundombinu ya shamba yenye thamani ya Milioni 32 yote hayo yakisimamiwa na Halmashauri pamoja na TAHA.
Picha ikionesha sehemu ya wanachama wa Lumolumo Women Group
Moja kati ya shamba la Lumolumo Women Group likiwa kwenye maandalizi ya kupanda mbegu
Sehemu ya shamba la mahindi linalomilikiwa na kikundi cha Lumolumo
Picha ikionesha sehemu ya miundombinu (NISHATI YA MWANGA WA JUA) inayowezesha wanakikundi wa Lumolumo kufanya shughuli zao za uzalishaji
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa