Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amesema Serikali itaendelea kuwapatia ushirikiano wakati wote, kuweka mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji wote ukizingatia kuwa haya ndiyo maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wote.
Hayo yamesemwa na Mhe. Mndeme alipotembelea na kuona namna ambavyo mgodi wa ZEM Develipment unavyofanya kazi zake katika eneo ambalo ni maarufu kama Mwakitolyo lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
"Nawapongeza sana uongozi wa mgodi huu wa ZEMD (mwakitolyo) kwa uwekezaji huu mkubwa sana ambapo kwakweli uwepo wa mgodi huu kumezalishwa ajira kwa wananchi ambao ni watanzania wenzetu zaidi ya 300, kuongeza mzunguuko wa fedha, kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa kupitia malipo ya kodi na kwa msingi huu serikali inawaahidi ushirikiano wakati wote", alisema Mhe. Mndeme.
Awali kupitia taarifa yao walisema wamepokea barua ya kuomba kujengewa vyumba vya madarasa matatu katika kata ya mwakitolyo, na kwamba wamepokea na watajenga kupitia sehemu ya fungu la fedha za mrejesho kwa jamii utokanao na mapato ya faida ya uzalishaji (CSR).
Kando na ahadi ya utekelezaji huo, pia Mhe. Mndeme aliuomba uongozi wa ZEMD kujenga pia nyumba kwa ajili ya waalimu ambao wanafundisha watoto wetu katika eneo hilo ili iende sambamba na ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa kama walivyoahidi, ombi ambalo lilipokelewa na kukubalika kutoka kwa uongozi wa ZEMD.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa