Wakulima wa Tumbaku katika Mkoa wa Shinyanga wamepata matumaini baada ya kuhakikishiwa soko la Tumbaku takribani kilo milioni 2 iliyokuwa imebaki kutokana na mnunuzi wa awali kushindwa kuendelea kununua.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Idd, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ulowa, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu katika ziara yake Mkoani Shinyanga mapema leo tarehe 20 Agosti, 2019 amesema Serikali tayari imepata mnunuzi mwingine anayeitwa "British American- BAT" na kibali chake kitakamilika muda wowote kuanzia sasa.
"Nimeambiwa kuhusu changamoto ya mnunuzi ilikuwa hajapata kibali, nimeongea na Waziri Mkuu na ameahidi ndani ya siku mbili tatu kibali kitakuwa kimekamilika, Serikali haina budi kuwasaidia wakulima wa Tumbaku kuhakikisha Tumbaku yao inanunulika" amesema Mhe. Balozi Seif.
Akizungumzia changamoto hiyo ya Tumbaku, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemueleza Mhe. Balozi kuwa, kampuni ya TLTC iliyokuwa inanunua Tumbaku kwa mkataba iliamua kutoendelea kununua lakini kuna kampuni ya "British Alliance" itanunua asilimia 10 Tumbaku hiyo.
"Hadi jana jioni tumepata taarifa kupitia Wizara ya kilimo kuwa, kampuni ya British American imeshapata barua ya kuwahakikishia kuja kununua Tumbaku yote iliyobaki Ushetu, hivyo msiwe na wasiwasi Tumbaku yote itanunuliwa" amesema Mhe. Telack.
Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa, amemueleza Mhe. Balozi kuwa, Wakulima wamebakiwa na Tumbaku haijanunuliwa hadi sasa hali inayochangia kudhoofisha hata mapato ya Halmashauri inayotegemea asilimia 80 kutoka kijiji cha Ulowa.
"Hayo mapato yakipotea na Halmashauri inalegea" amesema Mlolwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa