• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YATHIBITISHA VIFO VYA WATU SITA NA MAJERUHI 11 KATIKA AJALI YA MGODI WA MWAKITOLYO.

Posted on: May 18th, 2025

Na: Paul Kasembo – Mwakitolyo, Shinyanga DC

Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Anamringi Macha, imethibitisha kutokea kwa ajali katika mgodi wa dhahabu uliopo Kitalu Namba 8, Kijiji cha Nyaligongo Namba 2, Kata ya Mwakitolyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ambapo watu sita (6) wamepoteza maisha na wengine kumi na moja (11) kujeruhiwa.

RC. Macha alitoa taarifa hiyo Mei 18, 2025 alipowasili eneo la tukio na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo pamoja na familia zao, huku akisisitiza kuwa Serikali inatambua, inathamini na inaheshimu sana shughuli zinazofanywa na wachimbaji wadogo, na itaendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha usalama wao unalindwa wakati wote.

"Tumekuja kuwapa pole kwa niaba ya Serikali. Ninathibitisha kuwa jumla ya watu sita wamefariki dunia na wengine kumi na moja kujeruhiwa. Mmoja kati ya majeruhi hao ameshatibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani, huku wengine kumi wakiendelea kupokea matibabu hospitalini. Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa wahanga wa tukio hili," alisema RC. Macha.

Kwa ujumla, ajali hiyo ilitokea mnamo Mei 17, 2025 kuanzia majira ya saa 5:00 asubuhi, ambapo juhudi za uokoaji zilianza mara moja. Serikali inasisitiza kuwa idadi rasmi ya vifo na majeruhi ni kama ilivyotangazwa na si vinginevyo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo, sambamba na kuweka mikakati ya kuimarisha usalama na kuboresha mazingira katika shughuli za uchimbaji madini hususan kwa wachimbaji wadogo wote mkoani Shinyanga wakiwemo hao wa Mwakitolyo.

Picha zikionesha baadhi ya wachimbaji wakimsikiliza Mhe. Macha

Muonekano wa eneo la ajali ya mgodi

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • NATOA WITO KWA VIJANA HAPA SHINYANGA KUREJEA NA KUTATHIMINI UPYA NJIA ZA KUJIPATIA KIPATO - RC. MACHA

    May 20, 2025
  • SERIKALI YATHIBITISHA VIFO VYA WATU SITA NA MAJERUHI 11 KATIKA AJALI YA MGODI WA MWAKITOLYO.

    May 18, 2025
  • WAZAZI NA WALEZI, NENDENI MKAWE MABALOZI SAHIHI WA KAZI ZA MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN – RC. MACHA

    May 16, 2025
  • WAZAZI NA WALEZI WEKEZENI ZAIDI KATIKA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO – LYAMONGI

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa