Viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kutunga sheria ndogondogo kwa lengo la kuwabana wananchi wanaotumia maji ya kwenye madimbwi badala ya maji safi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Josephine Matiro wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji uliofanyika katika kijiji cha Manyada, Kata ya Usanda, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mhe. Matiro aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack katika uzinduzi huo, amewataka viongozi kutunga sheria hiyo ili wananchi wote watumie maji safi kutoka kwenye mabomba badala ya mito na madimbwi, ili kuepukana na magonjwa ya tumbo na kuhara.
Awali akisoma taarifa ya kamati ya watumiaji maji wa kijiji cha Manyada, Katibu wa Kamati hiyo Bw. john Daniel amesema kuwa changamoto kubwa ni wananchi kuendelea kutumia maji ya madimbwi na mito ambayo siyo salama na hivyo kuwa na hatari ya kupata magonjwa ya kipindupindu.
Aidha, ameeleza pia matumizi ya maji hayo yanakosesha kijiji fedha kwa ajili ya kuendeshea miradi ya maji ikiwemo matengenezo na Dizeli.
Aidha, Mhe. Matiro amewataka viongozi kuendelea kutoa elimu juu madhara ya kutumia maji ya kwenye madimbwi ili kulinda afya zao na kwa maendeleo ya mradi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa