Na. Shinyanga RC.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imefanya mafunzo elekezi ya kieletroniki ya mfumo wa MUKI kwa watumishi wake kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija Kata ya Ibinzamta huku Bi. Getruda Gisema akisema kuwa ujio wa mafunzo haya unakuja kurahisisha kazi na kupunguza gharama za uendeshaji.
kuanzia leo tarehe 15 mpaka 16 Septemba, 2023 kwa watumishi wa Manispaa katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija iliyopo katika kata ya Ibinzamata.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo haya Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi Getruda Gisema amewaeleza wataalami kuwa mafunzo haya yameletwa na Serikali kwa nia njema kabisa ambapo utendaji kazi kwa watumishi utarahisishwa sanjari na kupunguza gharama za matumizi mbalimbali ukizingatia mfumo huu ni wa kidigitali jambo ambalo linakwenda kuondoa matumizi ya shajala na kuanza kwa matumizo ya vishikwambi na kompyuta mpakato.
"Kupitia mfumo huu wa MUKI utaenda kusaidia watumishi kuweza kujua kanuni na maadili ya kiutumishi, majukumu yao ya kitaaluma na kujua stahiki zao mbalimbali pamoja na kujifunza mambo ya kiutumishi muda wowote na mahali popote kwa njia ya kieletroniki," alisema Gisema..
MUKI ni Mwongozo wa Mkufunzi wa Mfumo wa Ujifunzaji wa Kielekitroniki ambao kwa Manispaa ya Shinyanga mafunzo yamefanyika kwa siku mbili, yaani tarehe 15 na 16 Septemba, 2023 katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija.
PICHA NA MATUKIO
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa