Na. RS SHY - Tabora
MKOA wa Shinyangaa umeibuka kidedea katika michezo ya ufunguzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) ambayo yamefunguliwa Mjini Tabora ambapo yanafanyika kitaifa na kuhusisha Mikoa yote ya Tanzania.
Mkoa wa Shinyanga umeibuka kinara katika michezo ya mpira wa miguu (kundi maalumu) ambapo imeshinda 9 - 0 dhidi ya Katavi, mpira wa miguu Shinyanga imeshinda 1- 0 dhidi ya Songwe, mpira wa mikonno wasichana Shinyanga imeshinda 21 - 10 dhidi ya Rukwa pamoja goalball ambapo Shinyanga imeshinda 24 - 8 dhidi ya Kagera.
Mashindano haya amabayo yanahusisha michezo mbalimbali yamefunguliwa leo Juni 03, 2023 na Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Dkt. Charles Msonde.
Katika hotuba yake Dr. Charles Msonde amesisitiza juu ya uadilifu wakati wa michezo ya UMITASHUMTA mwaka huu wa 2023, ikiwepo udhibiti wa wanamichezo wasioruhusiwa (MAMLUKI) ili kuipa heshima sekta ya michezo mashuleni.
Akitoa maoni yake kuhusu michezo ya mwaka huu, Afisa Utamaduni Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Janeth Elias amewapongeza waandaji kwa maandalizi mazuri.
“Serikli kupitia waandaaji wamejitahidi sana kuboresha kila eneo, hii inaonyesha namna ambavyo vijana watayafurahia mashindano ya mwaka huu kwa kipindi chote watakachokuwa hapa Tabora, pongezi hizi ziende kwa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan” amesisitiza Bi. Janeth Elias.
Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA mwaka 2023, yanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mkoa wa Tabora ni mwenyeji wa mashindano haya kwa mwaka wa pili mfulululizo, ikiwa mwaka jana 2022 pia mashindano yaliandaliwa na Mkoa wa Tabora.
Picha ikionesha baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka Mkoa wa Shinyanga wakiwa uwanjani
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa