Na Johnson James, Shinyanga
Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la CSEMA chini ya ufadhili wa UNFPA, imeandaa semina ya siku mbili kuanzia Octoba 21-22 2025 kwa lengo la kujadili na kuimarisha uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto.
Semina hiyo imewakutanisha wajumbe wa kamati ya kusukuma mashauri kutoka ngazi ya Mkoa na Wilaya zote za Shinyanga, ikiwemo Mahakama, Polisi, TAKUKURU, Ustawi wa Jamii, na wadau wengine.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa, Lydia Kwesigabo amesema semina hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Haki Yangu, Chaguo Langu, unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia mpango wa MTAKUWWA.
Naye Mratibu wa Mradi huo, Jane Haule, amesema Mahakama na taasisi nyingine zina jukumu kubwa la kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa ukatili, hasa wanawake na watoto wenye ulemavu.
Semina hii imelenga kuimarisha ushirikiano wa wadau, kutatua changamoto za mashauri ya ukatili, na kuandaa mpango kazi wa pamoja wa kuboresha mnyororo wa utoaji haki mkoani Shinyanga.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa