Shirika la kijamii la "Women Fund Tanzania" lenye lengo la kuendeleza shughuli za utetezi wa haki za wanawake limetambulisha mradi wake katika Mkoa wa Shinyanga.
Akitambulisha mradi huo kwa uongozi wa Mkoa mapema jana tarehe 30 Mei, 2019 katika Hoteli ya Karena, Mkuu wa Program za miradi Bw. Carol Francis Mango amesema kuwa Shirika la WFT linawezesha utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) pamoja na mikakati mingine yote ya kutetea haki za wanawake.
Bw. Carol amesema, shirika hilo litaanza majaribio katika Halmashauri Wilaya ya Shinyanga na linajikita katika maeneo matatu ambayo ni utoaji wa ruzuku na uimarishaji wa uwezo wa wanawake, ujenzi wa mikakati ya kuimarisha mitandao ya wanawake na utafutaji wa rasilimali.
Naye Bi. Glory Mbia, Afisa mradi wa Shirika hilo amesema lengo la shirika ni kuchangia katika kujenga tapo la wanawake imara nchi Tanzania kwa kufadhili na kuimarisha uwezo wa wanawake kwa kuendeleza mikakati ya kunganisha nguvu za pamoja na kutafuta rasilimali.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bw. Boniphace Chambi, aliyekuwa mgeni rasmi wa utambulisho wa mradi huo amesema Serikali ya Mkoa na Wilaya ya Shinyanga itawapa ushirikiano wa kutosha shirika hilo ili liweze kutekeleza mradi.
Bi Glory Mbia, Afisa wa Shirika la WFT akitoa maelezo kuhusu mradi wa kuwezesha wanawake katika kutetea haki zao
Bw. Carol Mango akitoa maelezo kwa washiriki wa kikao kuhusu mradi wa WFT unavyofanya kazi katika kuwezesha shughuli za kuendeleza wanawake
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kutambulisha mradi wa WFT wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusu mradi huo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa