Na. Paul Kasembo, USHETU
WAZIRI wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (MB) amesema kuwa hatokuwa na msamaha kwa Mkandarasi yeyote atakayechelewesha kazi aliyopewa kwa kisingizio chochote kwakuwa upande wa Serikali kila kitu imewakamilishia ikiwemo fedha.
Mhe. Basungwa ameyasema haya leo tarehe 30 Novemba, 2024 alipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ikiwemo ya ujenzi wa Dadaraja la Kasenga (60m), Ubagwe (40m), Nh'wande (40m) na Mwabomba katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 18 huku akisisitiza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuboreshwa kwa miundombinu iliyoharibiwa na mvua za El - nino.
"Sintokuwa na msamaha kwa Mkandarasi yeyote atakayechelewesha kazi kwa singizio cha aina yoyote kwakuwa Serikali imekwishatekeleza sehemu yake kwnu wakandarasi ikiwemo fedha zenu, na katika hili sisi Wizara tutafuatilia na kusimamia kwa karibu zaidi kuona utekelezaji wake," amesema Mhe. Bashungwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa anamshukuru nakumpongeza sana Mhe. Rais kwa kuendelea kuipatia fedha Shinyanga ambapo kupitia Wizara ya Ujenzi imepata zaidi ya Bil. 18 ambazo zinakuja kuboresha na kuimarisha miundombinu Shinyanga jambo ambalo litawezesha muunganiko kuwa rahisi kwa Mikoa jirani ya Tabora na Geita.
Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ulikumbwa na athari ya kuharibika kwa miundombinu ya Barabara na Madaraja kutokana na mvua nyingi za El- nino, zilizonyesha takribani katika maeneo yote nchini. Kwa Mkoa wa Shinyanga, madaraja ya Ubagwe, Kasenga na Ng’hwande katika barabara ya Mwabomba – Igombe River na Nyandekwa – Ng’hwande katika jimbo la Ushetu wilaya ya Kahama yalipata madhara makubwa sana.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa