Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga Ndg. Donasian Kessy amesema kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Elimu (SEQUIP na EP4R) katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kishapu, na Manispaa ya Shinyanga.
Donasian ameyasema hayo Februari 4, 2025 wakati akitoa taarifa ya kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo ameongeza kuwa utekelezaji wa miradi hii uko katika hatua mbalimbali huku baadhi iko katika hatua ya manunuzi na mingine iko kwenye hatua ya umaliziaji.
“Tunaridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya elimu ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kishapu na Manispaa ya Shinyanga ambayo imefikia hatua mbalimbali ikiwemo ya umaliziaji,” amesema Donasian.
Kando na hayo amesema kuwa, TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha elimu ya kupinga rushwa inaendelea kutolewa katika Taasisi za Serikali, Binafsi na Wananchi kupitia kuanzisha Klabu za wapinga rushwa, mikutano ya hadhara, semina na vyombo vya habari lengo ni kuongeza uelewa na wigo wa mapambano dhidi ya rushwa.
TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga inatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa ikiwemo ya Sekta ya Elimu inakamilika kwa wakati, ufanisi na ubora uliokusudiwa na Serikali.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa