Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Shinyanga Bw. Donasian Kessy amesema kuwa TAKUKURU Mkoa imejipanga kuongeza uelewa kwa wadau kuhusu rushwa na madhara yake wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2024.
Kessy amesema haya wakati akizungumza na Wanahabari ofisini kwake amesema kuwa wanahakikisha wanatoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajumbe ambao ni wapiga kura za maoni, wagombea, wasimamizi wa uchaguzi na viongozi wa dini waandishi ambapo watajengewa uwezo na kupewa elimu pamoja na wananchi kwa Kata 130 za Mkoa wa Shinyanga.
"TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga tumejipanga vema kukuongeza uelewa kwa wadau kuhusu rushwa na madhara yake wakati uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2024 kwa Kata 130 katika Mkoa wote wa Shinyanga," amesema Kessy.
Kessy amesisitiza kuwa, elimu ya kutosha itatolewa kwa wananchi katika Kata hizo 130 ambapo itatolewa kwa njia ya Semina, vipindi vya redio, vikundi vya ngoma za asili na mikutanomya hadhara na kwamba TAKUKURU itachukua hatua za kisheria pale itakapobainika wagombea/wapambe wanajihusisha na vitendo vya rushwa.
TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga inaendelea kutoa wito kwa wananchi wote mkoani Shinyanga kuipatia ushirikiano na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
"Mtu yoyote akiona viashiria vya vitendo rushwa ATOE TAARIFA TAKUKURU kwa kufika Ofisi zao au kupiga simu namba 0738150196 au 0738150198 - Kahama, 0738 150199 - Kishapu au piga bure namba 113," amesisitiza Kessy.
"Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu;Tutimize Wajibu"
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa