Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amekabidhi gari kwa ajili ya matumizi ya Polisi Wilayani Kishapu baada ya gari lililokuwa likitumiwa awali kuharibika.
Gari hilo lenye thamani ya sh. Mil 80 aina ya Nissan limenunuliwa na Mgodi wa Mwadui na kukabidhiwa kwa Mhe. Telack kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mapema leo tarehe 18/10/2018.
Akikabidhi gari hilo, mhe. Telack amemtaka Mkuu wa Kituo hicho kulitumia kwa madhumuni ya kulinda usalama wa wananchi wa Kishapu.
Aidha, ameushukuru uongozi wa Mgodi wa Mwadui kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na Serikali ya Wilaya ya Kishapu hasa katika kuahidi kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi na kuomba wasichoke kwani nao ni jamii ya Wilaya hiyo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa