Na. Shinyanga RC
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameziagiza Halmashauri Mkoani Shinyanga kutenga vyumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea na kucheza watoto kwa wafanyabiashara wanawake wenye watoto wadogo wakiwa katika shughuli zao.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo alipotembelea, kukagua ujenzi wa vyumba vya biashara, kuzungumza na wafanyabiashara, kusikiliza pamoja na kutatua kero zao katika soko kuu la Manispaa ya Shinyanga.
Rc mndeme amesema kuwa, akina mama wanayo haki ya kuwa na faragha wakati wa kunyonyesha watoto wao jambo ambalo linapaswa kuzitekelezwa na Halmashauri zote katika masoko yote vyumba ambavyo vitatumika pia kuchezea watoto kwa kuwa ni salama na sahihi kwao.
"Naziagiza Halmashauri zote hapa Mkoa wa Shinyanga mtenge vyumba maalum vya faragha katika masoko yenu yote ili akina mama waweze kuwanyonyesha kwa faragha na kuwaacha watoto wao humo kucheza wakati wakiendelea na shughuli zao," alisema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze alimhakikishia Mhe. Mndeme kuwa maelekezo yote aliyotoa wameyapokea na watayafanyia kazi kwa haraka zaidi na kwa weledi mkubwa ili kuwatekelezea takwa hilo muhimu akina mama.
Mheshimiwa Mndeme amefanya ziara hii hapa Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuona maendeleo ya ujenzi wa vyumba 106 vya biashara katika soko kuu la Manispaa ya Shinyanga linalo gharimu zaidi ya Tzs. Bilioni 1.8 fedha zitokanazo na mapato ya ndani.
Picha mbalimbali zikionesha Mhe. Mndeme akiwa katika ukaguzi wa vyumba vya biashara pamoja na kuzungumza na wafanyabiashara katika soko kuu la Manispaa ya Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa