Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala ametoa siku 7 kwa Wakala wa Huduma za Misitu kuandaa na kuwasilisha mpango wa namna ambavyo watatekeleza suala la uvunaji wa mazao ya misitu nchi nzima kabla vibali havijatolewa.
Waziri Kigwangala ametoa agizo hilo wakati akihitimisha kilele cha maadhimisho ya upandaji miti Kitaifa ambayo Kitaifa yamefanyika katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mhe. Kigwangala amesema inatakiwa kuwe na utaratibu wa kutoa vibali kwenye maeneo ambayo yana rasilimali kwa kuzingatia kiasi cha rasilimali za misitu zilizopo.
Ameongeza kuwa, siyo vema kunatoa vibali wakati haijulikani uvunaji unafanywa wapi na kwa kiasi gani unafanyika. Hivyo lazima kuwe na mpango wa tathmini ya kila Mkoa una rasilimali kiasi gani. Amesema asipoupata mpango huo atasisitisha uvunaji. na kupeleka waraka kwa wakuu wa Mikoa wazuie uvunaji kwenye Mikoa yao.
“Natoa siku saba kwa TFS kuwasilisha kwangu mpango wa tathmini ya uvunaji wa mazao ya misitu nchi nzima kwa kuzingatia rasilimali za misitu kilichopo pamoja na kiwango halisi kitakachotakiwa kuvunwa ambacho hakitazidi robo ya rasilimali iliyopo”
“Lazima tutambue rasilimali tulizonazo, tujue tuna miti kiasi gani, ukubwa wake kiasi gani na akiba ya misitu ni kiasi gani na inavunwa wapi”. Anasema Kigwangala.
Katika hatua nyingine Dkt. Kigwangalla alitoa siku 30 kwa wananchi waliovamia ngitiri waondoke mara moja vinginevyo wataondolewa kwa nguvu huku akisisitiza wananchi wajifunze kilimo na ufugaji usioharibu mazingira.
Amewaasa wananchi kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na hali ya kupungua kiwango cha mvua baada ya vitendo hivi vinavyofanywa na binadamu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa