Na. Paul Kasembo, SHY RS.
TIMU ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa Grow Inreach katika Mkoa wa Shinyanga imetolewa wito wa kuongeza kasi ili kuepuka fedha kupitwa muda wa utekelezaji wake na hivyo kusababisha kurudishwa kwa wahisani huku ikisisitizwa kuunda Kamati ndogo itakayokuwa ikisaidia utekelezaji kati ya wanufaika/wananchi na Grow Inreach.
Haya yamesemwa leo tarehe 7 Mei, 2024 na Bi Alice Yugi ambaye ni Regionall Project Manager kutoka Ofisi ya World Vision Nchini Kenya wakati wa kikao kazi kati ya uongozi wa World Vision Kanda ya Ziwa na Timu ya utekelezaji wa mradi Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Dr. Yudas Ndungile Mganga Mkuu (M) Shinyanga.
"Pamoja na kuwapongeza kwa kupata mradi huu, lakini tunatoa wito kwa Timu inayohusika na utekelezaji wa mradi huu kuongeza kasi katika shughuli zake ili isijetokea sababu yoyote ya kuchelewesha mradi na kupelekea kurejeshwa kwa fedha za mradi," amesema Alice.
Mkoa kwa kushirikiana na Shirika la World Vision unatekeleza mradi wa Grow Enrich wa miaka mitano (2023 2027) mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Ujerumani na unatekelezwa kwenye Halmashauri ya Kiahapu na Shinyanga DC huku lengo la mradi ni kuboresha Afya na Lishe za vijana, wasichana, wanawake na wanaume wapatao 270,236 na kuimarisha usawa wa kijinsia kwenye maeneo ya mradi.
Hapa makundi lengwa ni pamoja na watoto wachanga miezi 0-6, miezi 6-23, Vijana na wasicha miaka 12-18 na watu wazima (wanaume na wanawake).
Kuzindua Mradi, uzinduzi rasmi wa mradi ulifanyika na ulihudhuriwa na viongozi wa serikali ya Mkoa na Halamashauri husika na viongozi wa ngazi ya jamii, uchambuzi wa uwezo wa wataalamu wa afya na kubaini mahitaji ya mafuzo kwa watoa huduma za afya.
Jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 28 vilifikiwa na watoa huduma 80 walifikiwa ambapo pia mradi ulifanya mafunzo kwa watoa huduma za afya 95 kwenye maeneo ya Lishe, Uzazi salama, GBV na ANC na utafiti wa awali ili kujua hali hali halisi ya viashiria vya mradi kabla ya kuanza rasmi kwa utekelezaji wa mradi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa