TUJIJENGEE UTAMADUNI WA KUFANYA USAFI - DC SAMIZI
Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi amewataka wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kujijengea utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya makazi, biashara na hata kazini wakati wote.
Mhe. Samizi ameyasema hayo leo tarehe 16 Sept, 2023 aliposhiriki Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani ambapo shughuli mbalinbali zimefanyika ikiwamo kushirikiana na wananchi, watumishi na wafanyabiashara katika kufanya usafi wa mazingira kwenye soko la Kambarage, pamoja na kutoa vifaa vya kuhifadhia tqka ngumu kwa soko hili la Kambarage, Miyumbani na Nguzo nane.
"Tujijengee utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yetu ili tuweze kuepuka na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya mlipuko kama vile kipindupindu," alisema Mhe. Samizi.
Maadhimisho haya ya Siku ya Usafi Duniani hufanyika kila mwaka ikikapo tarehe 16 Sept, ikiww na lengo la watu kufanya usafi katika maeneo yao mbalimbali ili kuendelea kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya mlipuko.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa