• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

TUMIENI MIKOPO HII KWA MIRADI MLIOKUSUDIA – DC MTATIRO

Posted on: April 2nd, 2025

#shinyanga_rs

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) @julius_mtatiro amewataka Wanavikundi ambao wamepokea Mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuitumia mikopo hiyo kwenye Miradi waliokusudia wakati wanaomba mikopo huku akiwasihi wairejeshe mikopo hiyo kwa wakati kwani mikopo hii ni ya hiari lakini urejeshaji ni lazima.

DC Mtatiro ameyasema haya leo Aprili 2, 2025 kwenye Hafla ya utoaji mkopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na yote amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze, Katibu Tawala  na Meya wa Manispaa ya Shinyanga kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ambayo yanasaidia katika uwezeshaji na utoaji wa mikopo hii ambayo inawanufaisha na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

“Ninawasisitiza wanavikundi ambao mmepata mikopo hii mkaitumie kwenye miradi ambayo mlikusudia kipindi mnaomba mikopo na msijaribu kuzitumia fedha hizo kwenye miradi mingine ambayo hamkuiorodhesha kwani kufanya hivyo ni kinyume cha kanuni na taratibu, lakini pia ninawasihi muirejeshe mikopo hii kwa wakati kulingana na muda ambao umewekwa kwani kukopa ni hiari lakini kurejesha ni lazima” amesema DC Mtatiro.

Aidha DC Mtatiro amewasihi wanavikundi ambao wamepata mikopo hii kuwasiliana na Maafisa Maendeleo ngazi ya Kata na katika maeneo wanayoishi kwa ukaribu pindi wanapopata changamoto kwenye urejeshaji wa mikopo ili waweze kusaidiwa na kutafuta suluhu za changamoto ambazo huenda wakapitia badala ya kusubiri mpaka watafutwe pindi wanaposhindwa kurejesha.

Kwa upande Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Peres Kamugisha akiwasilisha taarifa ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu amesema mpaka sasa wametoa takribani Mil. 255 kwenye Vikundi 19 ambapo 11 ni vya Wanawake, 7 vya Vijana na Kikundi 1 cha Walemavu huku akiendelea kusisitiza kuwa mikopo hii ni endelevu na itaendelea kutolewa kwenye vikundi ambavyo vitakidhi kanuni na taratibu.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa