Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuzitumia vema rasilimali zinazotuzunguuka katika maeneo yetu ili kuweza kuchechemua uchumi mtu binafsi, familia, Mkoa na Taifa kwa ujumla hjku akisisitiza kuwa kwa kutekeleza hili watakuwa wameishi na kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Imatisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) ambayo ipo chini ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Akifafanua rasilimali zinazotuzunguuka ni pamoja na Kilimo, Ufugaji pamoja na Uchimbaji wa Madini ili kuweza kuongeza thamani ya mnyororo kupitia rasilimali hizi huku akisisitiza uanzishwaji wa hata kiwanda kidoho cha kuzalisha na kiongeza thamani ya maziwa katika Mkoa wa Shinyanga ukizingatia tunao ng'ombe wengi sana kulinganisha na maeneo mengine.
"Niwaombe sana wananchi wa Mkoa wa Shinyanga twende kuzitumia vema rasilimali zote tulizonazo katika maeneo yetu ili tuweze kwenda na kuishi falsafa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia ambayo imekuja kuinua uchumi wetu kupitia fursa tulizonazo sisi," amesema RC Macha.
Kwa upande wake Bi. Sophia Mjema ambaye Mratibu wa Mabaraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kutoka Ofisi Rais Wanawake na Makundi Maalum amesema kuwa Serikali imeanza kuimarisha majukwaa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi hapa nchini kwa kuanzisha program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA).
Haya yote yakiwa na lengo kuu ni kuitambulisha programu hii, kuyafufua majukwaa uwawezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi ili waondokane na umasikini na kuingia katika uchumi wa kati kwa kufanya mapinduzi ya kiuchumi kwa kuhakikisha kunakuwa na bidhaa zinazeweza kuendeleza mkoa husika.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa