Na. Paul Kasembo, Msalala.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali itaendelea kushughulika na watumishi wachache ambao wasiokuwa waadilifu, wazembe na wenye nia ya kuharibu taswira nzima ya utendaji kazi wa Serikali.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 20 Mei, 2024 alikuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkurugenzi wa Msalala huku akiwataka watumishi kuwa waadilifu, kutumia lugha nzuri katika kuwahudumia wananchi na kuchapa kazi zaidi ili kumsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye maono yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maisha bora.
"Tutaendelea kuwashughulikia watumishi wachache wasiokuwa waadilifu na wazembe wenye nia ya kuichafua taswira ya Serikali, kwakuwa siyo kweli kwamba watumishi wote wanazo tabia mbaya kwa hili hapana hatuvumilia mtu", amesema Mhe. Macha.
Akiwasilisha taarifa ya utekeleza wa shughuli za maendeleo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ndg. Khamis Katimba pamoja na kumshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia Msalala fedha za maendeleo na na kuwahudumia wananchi.
Aidha Katimba amesema kuwa, Msalala imekuwa ni moja ya Halmashauri iliyopata Hati Safi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023, inaendelea kuimarisha na kuboresha utawala bora huku alisema kuwa Halmashauri imeishavuka lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 huku ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya ukomo wa kukusanya kwa mujibu wa Serikali.
RC Macha anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Shinyanga ambapo leo anaiangazia Halmashauri ya Wilaya ya Msalala katika sekta ya afya, utawala na baadae atazungumza na wananchi katika mkutano wa wananchi ambapo atajitambulisha, kupokea, kusikiliza na kutatua kero zao kweye viwanja vya Bugalama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa