Licha ya kuwa na mitambo ya kisasa na uwezo mkubwa wa kutoa mafunzo ya ufundi stadi, Chuo cha VETA Shinyanga kinadaiwa kushindwa kufikia jamii kwa kiwango kinachostahili kutokana na changamoto ya kutokujitangaza ipasavyo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita , alitoa wito huo wakati wa ziara yake chuoni hapo, akisisitiza kuwa chuo hicho kina fursa nyingi zinazoweza kuwainua wananchi kiuchumi endapo kitajitangaza vizuri.
Alisema mafunzo na huduma zinazotolewa na VETA hazipaswi kubaki ndani ya uzio wa chuo pekee, bali zinatakiwa kuifikia jamii kwa upana wake kupitia matangazo, ushiriki kwenye maonesho na kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha, Mhita alisisitiza kuwa VETA si mahali pa kutoa elimu ya ufundi tu, bali ni kituo muhimu cha kuchochea ubunifu, uzalishaji na ujasiriamali.
Alikitaka chuo hicho kutumia vizuri mitambo na wataalamu wake kuzalisha bidhaa zinazoweza kuuzwa na hivyo kusaidia kuongeza mapato ya ndani ya chuo.
Uongozi wa chuo uliahidi kuyafanyia kazi maelekezo hayo, huku ukiahidi kushirikiana na halmashauri na taasisi nyingine kuhakikisha VETA Shinyanga inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa vijana na jamii kwa ujumla.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa