Na. Paul Kasembo, KISHAPU DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametaka vijana mkoani Shinyanga kwenda shamba ambako ndipo kuna mafaniiio ya kweli, haraka na uhakika huku akikitolea mfano Kikundi cha Jipage kilichopo Kata ya Kishapu wilayani Kishapu ambacho kimeonesha mafanikio makubwa kutokana na kilimo.
RC Macha ameyasema hayo tarehe 13 Februari, 2025 alipotembelea Kikundi cha Jipage kinachoundwa na vijana 7 ambao wanajishughulisha na kilimo cha bustani ya Tikiti na ambao wametokea kuwa kivutio na mfano wa kuigwa kwa vijana wengine kutoka na mafanikio wanayopata kutokana na hiyo kazi.
"Vijana, niwatake sasa kubadilisha mtazamo na shughuli zenu na mjielekeze shambani ambapo huku mtapata mafanikio zaidi na ya kweli, ya haraka na henye uhakika kuliko kuendelea kubakia na mitazamo ya biashara za mijini zaidi," amesema RC Macha.
Akitoa salamu za kikundi Katibu wa jipage ndg. Samwel Abel alisema kuwa, kikundi kilianzishwa mwaka 2023 wakiwa vijana 13 ambapo walilima bustani na kupata takribani tikiti elfu kumi na moja (11,000) ambapo walipouza walifanikiwa kupata takribani Milioni 22 walipotoa gharama za uendeshaji walibakiwa na faida ya Milioni 11, na kwa mwaka 2014 walipata tikiti elfu 25 walipouza walipata Milioni 75 na baada ya kutoa hharama za uendeshaji walipata faida ya Milioni 48.
Pamoja na mafanikio mengine, lakini pia wameweza kununua shamba lao lenye ukubwa wa hekari 10, kulima tena takribani hekari 16 huku lengo likiwa ni kulima jumla ya hekari 30 na kwamba kwa sasa hali ya kiuchumi kwa familia zao zimetajwa kuimarika siku hadi siku.
Ziara hij ya Mhe. Macha katika Wilaya ya Kishapu imeangazia zaidi katika Sekta ya kilimo ambapo aliambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Victor Masindi, huku wataalam mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ndg. Emmanuel Johnson.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa