Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na Viongozi wa Kanisa la Moravian Mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Mchungaji Jonas Ludonya akiwa ameambatana na Mchungaji Upendo Kilongozi na Christian Malela (Mch) ambapo pamoja na wao kujitambulisha kwake lakini pia wamemkaribisha sana mkoani Shinyanga huku wakimuahidi ushirikiano wao wakati wote.
Kwa upande wake RC Macha amefurahi kukutana nao na kuwakaribisha zaidi wakati mwingine ofisini kwake huku akisema kuwa Serikali inathamini, inaheshimu na kutambua kazi zinazofanywa na madhehebu ya dini ikiwemo Kanisa la Moravian na kwamba itaendelea kushirikiana nao wakati wote kwa muktadha wa kuwahudumia wananchi ambao kimsingi madhehebu ya dini na Serikali wanamhudumia ambaye ni mwananchi.
@sizatumbo #shinyanga_rs
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa