Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela(katikati waliokaa) na washiriki wa mafunzo hayo
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela(katikati waliokaa) na washiriki wa mafunzo hayo
Mmoja wa Maafisa kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Tabora Bi. akitoa mada kuhusu sheria ya maadili ya viongozi katika mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akitoa neno la ufunguzi wa mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada kwa makini katika mafunzo hayo
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amewataka Viongozi wa Umma kufuata sheria na misingi ya maadili inayowaongoza katika utendaji wao bila kuingiza maslahi yao binafsi.
Msovela ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya maadili na mgongano wa kimaslahi kwa wajumbe wa Kamati za maadili ya Viongozi wa Umma Mkoa wa Shinyanga, yaliyofanyika kwa siku moja katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga hapo jana tarehe 17/12/2019.
Amewataka Viongozi hao watafakari kwenye Taasisi wanazozisimamia ni changamoto zipi wanakutana nazo ili wazifanyie kazi na kupunguza migogoro na kutatua matatizo katika utumishi wa Umma.
Amesema wajikumbushe wajibu wao katika kila nafasi waliyonayo ikiwemo maamuzi wanayoyatoa bila kuathiri maslahi ya Taifa.
Katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na Wakuu wa Idara wa baadhi ya Taasisi pamoja na Madiwani, mada za sheria ya maadili ya viongozi wa Umma, Mgongano wa Kimaslahi na Kanuni za maadili na utendaji katika utumishi wa Umma ziliwasilishwa na Maafisa wa Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa