Na. Paul Kasembo, Kakola - Msalala.
MKUU aa Mkoa aa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametaka waajiri hasa wa Sekta binafsi kuwaruhusu waajiriwa wao ili waweze kujiunga na Chama cha Wafanyakazi chochote ili waweze kunufaika na kuzisaidia sekta zenu kwakuwa ni wajibu na haki kwa pande zote mbili.
Maelekezo haya yametolewa na RC Macha wakati akihutubia wafanyakazi wa Mkoa wa Shinyanga katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambayo kwa Mkoa wa Shinyanga sherehe zilifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kakola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo pamoja na mambo mengine RC Macha aliwaeleza watumishi kuwa suala la Kikokotoo limekwishapokelewa na Serikali na litafanyiwa kazi ukizingatia kuwa limesemewa na Mamlaka mbalimbali.
"Pamoja na kuwapongeza kwa maadhimisho haya leo, nchukue nafasi kuwaelekeza waajiri wote wa Sekta binafsi kuwaruhu watumishi wao kuchagua Chama cha Wafanyakazi chochote na kujiunga kwakuwa ni haki yao nanyi ni wajibu wenu kutekeleza hili," amesema RC Macha.RC
Aidha, RC Macha amewaahidi wafanyakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa yale yote yaliyosemwa na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Mkoa ameyachukua na kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wake atayatekeleza haraka na kwa ufanisi zaidi, na kwa yale yaliyo juu ya mamlaka yake ameahidi kuyafikisha tena kwa maandishi bila kupunguza neno lolote.
Kuhusu suala la Kikokotoo, amesema kuwa ni jambo ambalo kwa hivi karibuni limesemwa na mamlaka mbalimbali na hivyo anayoimani kubwa na Serikali kuwa litafanyiwa kazi na pande zote zitakuwa sawa kabisa kwakuwa Serikali hii ni sikivu sana.
Kwa upande wake Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Shinyanga alisema kuwa suala la Kikokotoo limekuwa likidhoofisha watumishi sana na hivyo akaiomba Serikali kulifanyia kazi huku akisistiza juu ya vifurushi vyenye maslahi zaidi ka wafanyakazi ili kuongeza ari ya watumishi kufanya kazi zaidi.
Mwaka 1886, vyama vya wafanyakazi vya Marekani vilianzisha mgomo wa watu wengi kudai kufanya kazi saa nane kwa siku , kwa kuzingatia wazo la mwanamageuzi wa kijamii wa Uingereza Robert Owen.
HABARI PICHA
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati wa sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI - KALOLA, MSALALA.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa