Waandishi wa Habari wametakiwa kutoa habari sahihi kwa wananchi ili kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa wasia huo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani ambayo Kimkoa yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Liga, Manispaa ya Shinyanga.
Mhe. Telack amesema, waandishi wa habari wakitumia kalamu zao vizuri kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari, Mkoa na nchi kwa ujumla patakuwa ni mahali salama kwa kila mwananchi na hata wageni.
Aidha, amewataka waandishi wa Habari kuwa na mtazamo wa kujitegemea kwa kubuni shughuli za kiuchumi kwa umoja wao ili kuongeza vipato vyao na waepukane na tabia ya kutumika kinyume na maadili ya kazi yao.
Nao baadhi ya wadau wa Habari Mkoani Shinyanga wamewataka waandishi wa Habari kuwa wakweli kwa kuandika habari zenye kulenga kuelimisha jamii kuliko kutumia muda mwingi kuandika habari zisizosaidia wananchi.
Katika maadhimisho hayo, wadau hao kwa pamoja wamekubaliana kukutana angalau mara mbili kwa mwaka ili kukumbushana masuala mbalimbali ya kusaidia jamii na Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa