Wadau wa afya Mkoani Shinyanga wametakiwa kujenga dhana ya ushirikishaji katika ngazi zote za kutekeleza majukumu yao ili kuwa na lugha moja na Serikali ya Mkoa kwa kuwa na taarifa zenye takwimu sahihi.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amesema wakati wa kikao cha pamoja cha siku mbili cha wadau wa afya Mkoani hapa kuwa, dhamira kubwa ya Serikali ya Mkoa ni kuzungumza lugha moja kwa upande wa sekta ya afya.
"Dhamira kubwa ya Sekretarieti ya Mkoa ni kuzungumza lugha moja kwa upande wa sekta ya afya, tuwe na takwimu tunazozifahamu kwa pamoja kabla hazijapelekwa popote na ziwe na utaratibu unaoeleweka" amesema Msovela.
Msovela amesema kuwa, endapo wadau wote watafanya kazi kwa pamoja matokeo ya kazi hizo yataonekana kwani kuna baadhi ya maeneo yanayofanyiwa kazi bado mambo hayaendi kadri Serikali inavyotaka.
Amesema wadau wapo wengi lakini sehemu moja inakuwa na wadau zaidi ya mmoja hali inayopelekea kuingiliana katika majukumu hivyo Serikali imeona iingilie kati na kuwaagiza wadau wote kuripoti kabla ya kufanya kazi na kupangiwa maeneo.
Mkoa wa Shinyanga una wadau wa afya zaidi ya 30 ambao wamekaa kikao hicho kwa lengo la kutambuana na kujadili masuala ya afya kwa pamoja na namna ya kukabili changamoto zilizopo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa