Na. Paul Kasembo, KISHAPU.
WADAU wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wadau wa Maji wilayani Kishapu ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Kishapu ambao Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude wameazimia kwa pamoja kulipa madeni yote wanayodaiwa na RUWASA ndani ya siku 30 kuanzia sasa huku kundi kubwa likilengwa na kutajwa kuwa ni Taasisi za Serikali zikowemo za Elimu na Afya.
Haya yameazimiwa leo tarehe 23 Agosti, 2024 katika mkutano huu ambao umejumuisha wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, wakuu wa Divisheni, Vitengo, Kamati ya Usalama Wilaya na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu akitoa wito na angalizo kwa Mkuu wa Shule au Mganga kwenye taasisi yake ambayo inadaiwa kuhakikisha inalipa madeni hayo haraka na vinginevyo atapaswa kujitathimini kama anatosha kwenye nafasi yake.
Awali akitoa taarifa ya RUWASA Wilaya ya Kishapu Injinia. Dickson Kamanzima amesema kuwa, moja kati ya jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora yenye kuwafikia wanachi kwa maji safi na salama wakati wote huku akitoa wito kwa wadau wengine kusapoti juhudi hizi kwakuwa wao peke yao hawawezi kulifanikisha hili kwani maji ni uhai.
Katika salamu zake Mwenyekiti wa mkutano huu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu amewaeleza wananchi kuwa Wadau wote wa mkutano huu wanalo jukumu kubwa la kuendelea kuelimisha jamii zetu katika maeneo tunayotoka juu ya matumizi sahihi ya maji safi na salama ikiwa ni pamoja kutunza vyanzo vya maji, kulipia ankara za maji kwa wakati na kuacha tabia ya kushawishi wananchi kuacha kuyatumia maji ya visima ili waweze kuletewa maji ya Ziwa Victoria kwani wakati ukifika maji hayo yatawafikia hata bila mgomo huu.
"Niwaombe wadau wote wa mkutano huu wa mwaka twende tukatekeleze jukumu hili muhimu la kuelimisha jamii tunayoishi nayo huko tunakotoka juu ya umuhinu wa matumizi sahihi ya maji safi na salama na pia watunze vyanzo vyote vya maji ili tuendelee kunufaika navyo," amesema
Injinia Dickson Kamanzima akielezea jambo wakati wa mkutano wa wadau
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa