Na. Paul Kasembo, KAHAMA DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa wananchi kiongeza utayari na uhiari wa kulipa Kodi huku akiwasisitiza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendeleza uaminifu, uzalendo na ufanisi zaidi katika utekelezaji wao wa majukumu ili kuendelea kufikia lengo lao kwa mwaka pasipokuwa na malalamiko na kero kwao jambo ambalo litawapelekea wafanyabiashara kuwa na ukaribu sana na TRA.
RC Macha ameyasema hayo wakati akiongoza Hafla ya Utoaji Tuzo ya Mlipa Kodi kwa mwaka 2023/2024 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malex ulipo Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Meneja TRA Mkoa wa Kikodi Shinyanga ndg. Emmanuel Maro na Meneja wa TRA Mkoa wa Kikodi Kahama ndg. Warioba Kanire, wafanyabiashara na wananchi.
"Wafanyabiashara, niwaaombe sasa muongeze utayari na uhiari katika kulipa kodi ili Nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo na kuwaletea huduma zote stahiki wananchi, nanyi TRA endelezeni uaminifu, uzalendo na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yenu katika kuwahudumia wananchi ili muendelee kufikia lengo kusudiwa pasipokuwa na malalamiko wala kero kutoka kwa wafanyabiashara jambo ambalo litawapelekea wqo kuwa karibu na TRA, amesema RC Macha.
Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa yeyote yule asiyetoa stakabadhi kwa mnunuzi anayenunua bidhaa na yjle asiyedai wala kuchukua stakabadhi kutoka kwa muuzaji wote hao wanakuwa wanalihujumu Tiafa na siyo wapenda maendeleo kwani kila mmoja akitekeleza wajibu wake anakuwa anasaidia maendeleo kwa Taifa na kuinua uchumi wa wananchi wote kwakuwa mapato yataingia Serikalini na hivyo kupelekea lengo kuu la kufukiwa ambalo ni kuwapelekea maendeleo na huduma zote muhimu wananchi na kujenga imani kubwa wa Serikali yao.
Akitoa salamu za Mamlaka kwa niaba ya Kamishna wa TRA Tanzania ndg. Emmanuel Nnko ambaye pia ni Mkurugenzi wa TEHAMA TRA - Kahama alisema kuwa hafla hiyo ni kielelezo cha kutambua, kuthamini na kuheshimu mchango mkubwa wa walipa kodi kwa Mkoa wa Kikodi Kahama na Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa