Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaagiza waajiri wote ndani ya mkoa wa shinyanga kuhakikisha wanasimamia stahiki zote za makatibu mahsusi huku akisisitiza kuwa yeyote anayewabeza na kuwadharau makatibu mahsusi huyo hajitambui.
Agizo hilo amelitoa leo tarehe 7 Desemba, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha kuzindua Chama cha Makatibu Mahsusi (TPSEA) mkoa wa Shinyanga mara baada ya kupokea risala ya wanachama hao ambapo ndani yake ilielezea changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa stahiki zao kama kuhudhuria mafunzo na mikutano mbalimbali inayohusu taaluma yao.
"Nimesikiliza kwa makini risala yenu nichukue nafasi hii kuwaagiza waajiri wote kusimamia stahiki za makatibu mahsusi ikiwemo kutenga bajeti ya kuhudhuria mafunzo na mikutano mbalimbali inayohusua taaluma yao pamoja na kuwapatia ruhusa ya kushiriki mafunzo na mikutano hiyo huku akimuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumho kusimamia utekelezaji wa maagizo haya." amesema Mhe. Mndeme
Aidha, Mhe. Mndeme ameendelea kusisitiza kuwa makatibu mahsusi ni watu muhumu sana katika ofisi wanabeba siri nyingi pamoja na kujua mambo mengi yanayohusu ofisi, mtu akiwadharau makatibu mahsusi basi mtu huyo atakuwa hajitambui.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mndeme amewasihi makatibu mahsusi kupata muda wa kujiendeleza vizuri kielimu ili wawezi kuwa viongozi mbalimbali Kitaifa
Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) kina jumla ya wanachama 118 kutoka Taasisi za Serikali na umma Mkoani Shinyanganga.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa