Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mne. Anamringi Macha amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Shinyanga kuhakikisha kuwa viongozi waliochaguliwa wanapewa Semina ya Uongozi kwa wachaguliwa wote katika nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa, Kijiji, Kitongoji na Wajumbe wao kabla ya Januari 2025.
RC Macha ameyasema haya wakati akishuhudia Uapisho wa viongozi hao tarehe 29 Novemba, 2024 hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano uliopo Shule ya Sekondari Shinyanga Wasichaa hapa Manispaa ya Shinyanga ambapo takribani viongozi 570 wameapishwa.
"Ninawaelekeza Wakurugenzi wote wa Halmashauri zilizopo hapa mkoani Shinyanga kuhakikisha mnawapatia Semina viongozi hawa wote waliochaguliwa kabla ya mwezi Januari 2025 ili waweze kufanua kazi vema kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo na hii kwa wote, " amesema RC Macha.
Kando na maelekezo haya, RC Macha pia amewatahadharisha viongozi hawa kuwa, hatasita kumuondoa yeyote kwenye nafasi aliyoipata punde atakapobaini ukiukwaji wa utendaji kazi wake na kwamba uchaguzi mdogo utafanyika wakati wowote kupata kiongozi mwingine ambaye atakuwa tayari kuwatumikia wananchi wetu.
Uapisho kwa Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wao unafuatia kukamilika kwa Uchaguzi wa Serikaki za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 nchini kote.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa