Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini wameagizwa kuhakikisha kuwa, wafanyabiashara walionunua vitambulisho vilivyotolewa na Serikali kwa shilingi elfu 20 hawatozwi kodi yoyote kwa mwaka mzima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mapema jana tarehe 03/03/2019 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama, alipokuwa anakamilisha ziara yake ya kikazi Mkoani Shinyanga.
Mhe. Samia amesisitiza kuwa, Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote atakayebainika anawatoza ushuru wafanyabiashara wadogo waliotambuliwa na Serikali atatoa maelezo ya sababu za kufanya hivyo kwani
Amesema vitambulisho hivyo ni kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ambao mtaji wao hauzidi shilingi milioni 4 hivyo wakishanunua kwa sh. Elfu 20 hawatakiwi kulipa kodi yoyote kwa mwaka mzima.
“Lengo la Serikali ni kulenga kundi ambalo halitahusika kwenye kodi ya biashara,wenye mtaji wa milioni nne kushuka chini kwa mwaka ndiyo wachukue vitambulisho” amesema Mhe. Samia.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa