• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI, TOENI USHIRIKIANO KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA - DC MKUDE

Posted on: December 10th, 2024

Na. Paul Kasembo, Kishapu.

MKUU wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amewaasa wananchi wa Kata ya Shagihilu na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla kushirikiana na vyombo vya dola kuripoti taarifa sahihi na haraka wanapoona matukio ya ukatili wa kijinsia yakitokea katika maeneo wanayoishi ili kuhakikisha wanapunguza na kutokomeza ukatili unaofanyika na kuifanya jamii ibaki salama.

DC Mkude ametoa wito huu leo tarehe 10 Desemba, 2024 wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia mkoani Shinyanga akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, maadhimisho ambayo yamefanyika katika Shule ya Msingi Shagihilu iliyopo Kata ya Shagihilu Wilaya ya Kishapu yakiwa na Kauli Mbiu isemayo “Kuelekea Miaka 30+ ya Beijing: Chagua Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia”.

“Serikali inaendelea na jitihada za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Mkoa wetu lakini ombi langu kwenu wananchi ni kwamba muwe tayari kushirikiana na vyombo vya dola kwa kuripoti na kutoa taarifa sahihi haraka mnapoona au kusikia matukio ya ukatili yanafanyika katika maeneo yenu kwani lengo letu sote ni moja kuhakikisha tunakomesha kabisa matukio haya na kuifanya jamii yetu iwe sehemu salama zaidi” amesema DC Mkude.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Lidya Kwesigabo akiwasilisha taarifa juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Mkoa wa Miaka Mitano wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto amesema, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali wameshiriki na kuhamasisha utoaji wa elimu ya ukatili dhidi ya watoto mashuleni, kutoa huduma ya msaada wa kisheria pamoja na kuunda madawati ya ulinzi wa mtoto ili kuzuia matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Maendeleo ya Watu na Afya Tanzania (TDHS) kwa mwaka 2022 matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Shinyanga yalipungua na kufikia asilimia 28 ukilinganisha na mwaka 2010 ambapo ilikuwa ni asilimia 34, lakini pamoja na yote jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha matukio haya yanapungua kwa kuleta huduma za kijamii.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa