MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaasa wananchi kwenda kutumia vizuri na kikamilifu chandarua katika makazi yao ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria huku akisisitiza kuwa Serikali imetekeleza sehemu yake ya kugawa vyandarua wananchi wake wote wakiwemo wa Mkoa wa Shinyanga na iliyobakia kwa sasa ni wananchi kuchukua bure na kwenda kutumia bila malipo yoyote.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 8 Februari, 2025 wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua hafla iliyofanyika Kata ya Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko, viongozi wa vyama vya siasa na wananchi.
Mkoa wa Shinyanga unatarajia kugawa takribani vyandarua 1,555 vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni 12 na lengo la Serikali ni kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya Mpango wa Taifa wa Kupambana na Kuthiniti Ugonjwa wa Malaria (NMCP)
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa