Wananchi wametakiwa kuacha kupeleka kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Mikoa malalamiko yanayolenga mashauri ambayo tayari yapo mahakamani.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Sheria leo tarehe 06/02/2020, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewaeleza wananchi kuwa, Serikali haifanyii kazi mashauri hayo kwa sababu tayari yanashughulikiwa na mahakama ambayo ndiyo yenye majukumu ya kupokea na kutatua mashauri.
Mhe. Telack amesema kuwa, Serikali inashirikiana kwa karibu na mahakama kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote. "Nikiwa nafahamu kuhusu shauri ambalo lipo mahakamani nitawasiliana na Jaji na kumpa dondoo kuhusu shauri hilo ili aweze kupata mwanga na kufanya maamuzi kwa usahihi"
Akifafanua suala la baadhi ya watu kulalamikia watu kuwekwa ndani na Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Telack ametoa wito kwa wananchi kuwa, hakuna mwananchi aliye juu ya sheria hivyo, mtu yeyote anayevunjwa sheria atawajibishwa. Telack amefafanua kuwa, nafasi za Wakuu wa Wilaya na Mikoa ni za Serikali hivyo wanasimamia shughuli zote ndani ya maeneo yao husika na iwapo wananchi wakiona mtu kawekwa ndani basi kuna jambo amefanya.
"Kuna mahali lazima Serikali itumie nguvu, ukisikia mtu kawekwa ndani na Mkuu wa Wilaya au Mkoa ujue lipo jambo amelifanya, kama kuna dalili za uvunjifu wa amani lazima hatua zichukuliwe, mengine tusipoyafanya hata nyie wananchi yanawaathiri" amesisitiza Telack.
Awali akitoa neno kwa niaba ya Chama cha Wanasheria Kanda ya Shinyanga Bw. Mbatina ameshauri Serikali iongeze rasilimali watu kwenye Mahakama ili kutatua tatizo la mashauri kuchukua muda mrefu kumalizika.
Mbatina amesema kuwa, Mahakama ina wajibu wa kuhakikisha mashauri yanayopelekwa yanamalizika kwa wakati na kwa haraka.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiingia katika eneo la maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoa wa Shinyanga, Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga akiwa ni mgeni mahususi
Mawakili, Wanasheria na Mahakimu wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano kuadhimisha siku ya Sheria
Maandamano yakiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga Mhe. Gerson Mdemu kuelekea eneo la maadhimisho
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga Mhe. Gerson Mdemu, akikagua gwaride maalumu kwa ajili ya siku ya Sheria katika viwanja vya Mahakama Kuu Mjini Shinyanga
Shekh Soud Kategile, kwa niaba ya Shekh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiomba dua kabla ya kuanza shughuli za maadhimisho ya siku ya Sheria
Askofu Emmanuel Makala wa Kanisa la KKKT akiomba kabla ya kuanza shughuli za maadhimisho ya siku ya sheria
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akicheza pamoja na wanakwaya wa Kanisa la AICT Kambarage Shinyanga wakati wakitumbuiza siku ya Sheria Mkoani hapa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Sheria kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akicheza pamoja na kikundi cha Shinyanga Artist wakati wakitumbuiza siku ya Sheria
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa