Watendaji wa Vijiji na kata Mkoani Shinyanga wameagizwa kuhakikisha akina mama wajawazito wanajifungulia kwenye vituo vya afya na kutoa taarifa kila mwezi kuhusiana na vifo vinatokanavyo na uzazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa agizo hilo mapema leo tarehe 18 Januari, 2019 katika Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vinatokanavyo na uzazi.
Katika uzinduzi wa Kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya “Jiongeze, tuwavushe salama”, Mhe. Telack amesaini mikataba ya utekelezaji na uwajibikaji wa Kampeni hiyo pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoani hapa.
Mhe. Telack amesema kuwa, Watendaji wa vijiji na kata ndiyo wenye uwezo wa kuwafahamu akina mama wajawazio waliopo kwenye maeneo yao, hivyo ni rahisi kuweza kuwafuatilia endapo kutatokea vifo na kutoa taarifa na sababu za vifo hivyo kwenye ngazi ya Halmashauri hatimaye Mkoani.
Amewataka Viongozi na watendaji wote waliohudhuria katika uzinduzi huo kufikisha elimu hadi vijijini juu ya umuhimu wa akina mama wajawazito kupata huduma katika vituo vya afya.
Aidha, amewaomba pia viongozi wa Dini na Siasa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi waelewe umuhimu wa kuwatunza wajawazito.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa