Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Daktari Yudas Ndungile kuwa watoto wakilelewa katika misingi inayotakiwa itawapunguzia mzigo Jeshi la Polisi katika suala la uhalifu kwani watakuwa na maadili na kimsingi wanapaswa kuanza kulelewa wakiwa bado wadogo.
Dr. Ndungile ameyasema haya wakati wa ufunguzi wa kikao cha tathimini za Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga zikilenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ili kufikia ukuaji timilifu wa watoto.
"Watoto watakapolelewa kwenye misingi inayotakiwa itawezekana kuwapunguzia mzigo Jeshi la Polisi katika suala la uhalifu kwani wanatakiwa waanze kulelewa wakiwa bado wadogo," amesema Dr. Ndungile.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Lyidia Kwesigabo amesema katika maazimio matano waliyojiwekea watahakikisha wanayafanyia kazi na kuyaboresha ikiwemo kushirikisha taasisi binafsi katka kuwalinda watoto na kuwapatia miundombinu rafiki.
Aidha, Maaifsa ustawi wa jamii kutoka halmashauri zote waliwasilisha tathimini katika maeneo yao ikiwa programu ya (MMMAM) ilizinduliwa rasmi kwenye halmashauri hizo mwezi Februari mwaka huu.
Kando nao, mwakilishi kutoka Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto nchini (TECDEN ) Ndg. Christopher Peter amezipongeza Halmashauri zote kwa kuanza kupiga hatua katika utekelezaji wake, huku akisistiza uwajibikaji zaidi.
HABARI PICHA
Dr. Yudas Ndungile
Bi. Lydia Kwesigabo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa