#shinyanga_rs
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema ipo haja kwa watumishi mkoani hapa kuweka umuhimu zaidi kwenye bima huku wakitakiwa kufuata ushauri wa madaktari ili waepukane na magonjwa nyemelezi.
Mhe. Mtatiro ameyasema hayo Februari 24, 2025 wakati akifungua Mafunzo kwa watumishi yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ambayo pamoja na mambo mengibe yalilenga kuwajengea uelewa wa Bima ya maisha, gari, nyumba na mali nyinginezo.
"Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, niseme tu kwamba kuna kila sababu ya kuweka umuhimu zaidi kwenye masuala yote yanayohusu Bima na kwa kuzingatia ushauri wa wataalam ili kuepukana na magonjwa nyemelezi,h amesema Mhe. Mtatiro.
Kwa upande wake Kamishna wa Bima nchini Dkt. Baghayo Saqware amewataka watumishi mkoani Shinyanga kujenga utamaduni wa kukata bima ya kulinda mali zao ikiwemo Mazao, Madini, Viwanda na gari jambo ambalo litawaepusha na hasara ya mali pale majanga yanapotokea ikiwemo mali zao kuungua moto au kusombwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa.
Dkt. Baghayo amesema kuwa, utafiti uliofanywa na Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) umebainisha kuwa licha ya wananchi kutokuwa na uelewa wa kukatia bima mali zao, lakini pia hata watumishi nao wanakumbwa na hali hiyo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa