Na, Shinyanga RS.
Mrajis MSaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 5 amekabidhi Leseni ya daraja “B” kwa Mwadui SACCOS na Cheti cha usajili kwenye mkutano wa wanachama wa Mwadui SACCOS. Ambao umehudhuriwa pia na Mmiliki wa Mgodi ambae pia ni mwajiri wa watumishi hawa Bw. Isack Mtoni Gamba.
Pamoja na kuwakabidhi Leseni yao ya biashara na cheti lakini pia amewapongeza Bodi iliyopo kwa kushirikiana na wanachama wake kwa kuonesha ushirikiano mkubwa wakati wa ufufuaji wa chama hiki.
Chama hiki cha akiba na mikopo cha watumishi wa Mwadui SACCOS kilianza mgogoro tangia Mwaka 2013 baada ya uongozi wa chama kufuja pesa za wanachama wake na kupelekea chama kushindwa kutoa mikopo na hata mikopo kwa wanachama wake. Mwaka 2017 baada ya uliokua uongozi wa bodi kutosimamia chama hiki kwa uamini na uadilifu na kupelekea fedha za wanachama kupotea.
Ofisi ya Mrajis kwa kushirikiana na Afisa ushirika na Uongozi wa bodi imeanza harakati za kusaidia kufufua SACCOS hii tangia mwaka2021 kwa kuondoa uongozi uliokifikisha chama kwenye hasara hii baada ya kufanyika kwa uchunguzi na kubaini madeni hayo.
Tume ya maendeleo ya ushirika Nchini katika kuhakikisha madeni haya yanarejeshwa imemleta mkusanya madeni ambae hivi sasa ameanza kazi rasmi na atashirikiana na uongozi mpya ili kusaidia madeni hayo kurejeshwa ili kuongeza mtaji wa chama. Ofisi imeendelea kuhamasisha wanachama wake kuona namna bora ya kuweza kukusanya madeni hayo na kuwashawishi kushirikiana kufufua SACCOS yao.
“Lakini pia tunamshukuru mwajiri wao kampuni ya Williumson ya Mwadui kukiwezesha chama hiki na kuonesha nia ya kukisaidia ili kiweze kusimama Kwakua watumishi hao wa mgodi walionesha umuhimu wa kuwa na SACCOS katika eneo la kazi itakayowasaidia kukidhi mahitaji yao ya kifedha na kwa riba nafuu kwa wakati wowote ambao mtumishi anaweza kupata shida kama ilivyokua hapo awali,” alisema Hilda.
Bi. Hilda alieleza sababu ya vyama vingi vya akiba na mikopo kufa ni kitokana na uongozi mbovu, kukosekana kwa sera na mikataba isiyozingatia sheria ambayo mala zibgia inatoa miaya ya viongozi wasiokuwa waadirifu kutumika vibaya.
Hivyo aliwataka wanachama wafahamu kuwa wao ndio wanalojukumu la kuusimamia na kuulinda ushirika wao na sio kuiachia bodi. Huku akisema kuwa wao kama wasimamizi jukumu lao kuu ni kuhakikisha uendeshaji wa shughuli za chama unazingatia sheria , kanuni na taratibu zote ili kuwezeaha ushirika kuwa endelevu.
Hivyo wanachama wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha ushirika huu ambao umesinzia kwa muda mrefu unaimarika na unakidhi mahitaji ya kuanzishwa kwake na sio kuwafaidisha wachache.
Mwenyekiti wa bodi Bw. Shija Shilagi Golani aliwaomba wanachama kushirikiana wa kutosha na mkusanya madeni aliyeletwa na Tume ya maendeleo ya ushirika kwa kipindi hiki ili aweze kutuangalizia fedga zetu.
“Na kumuomba mwajiri atusaudie kwa wale wadaiwa ambao wanamalipo yao kwenye ofisi basi waweze kukatwa na fedha hiyo iingie kwenye akaunti ya chama,”alisema Golani.
Picha ikionesha sehemu ya wana SACCOS MWADUI wakati wa kikao cha kupokea Leseni na Cheti
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa