WAZIRI wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amezindua mradi wa upanuzi wa mtandano wa maji katika kijiji cha malenge kata ya isagehe manispaa ya Kahama mkoani shinyanga, mradi ambao umegharimu aaidi ya Tzs. Mil. 940 utakao huhudumia takribani watu elfu 15 katika kata hii na maeneo jirani.
Akizingumza baada ya kuzindua mradi huu tarehe 9 Jan 2024, pamoja na mambo mengine, lakini Mhe. Aweso ameipongeza sana Mamlaka ya Maji Wilayani Kahama (KUWASA ) kwa kusimamia vyema mradi huu huku akiagiza Mamlaka hii kuanza mchakato wa kutafuta eneo ili kuanza ujenzi wa bwawa maalum litakalo saidia kutatua tatizo la maji pindi itokea hitilafu kwenye Ziwa Viktoria ambapo ndio chanzo kikuu cha maji kwa Wilaya ya Kahama.
Amesema kwa sasa Wilaya nzima ya Kahama inategemea chanzo kikuu kimoja cha maji cha Ziwa Viktoria na kutokuwapo kwa chanzo mbadala kusababisha tatizo la maji kuwa kubwa pindi inapotokea hitilafu kwenye chanzo hicho. Hivyo ameiagiza KUWASA kushirikiana na uongozi wa wilaya kutafuta eneo na kujenga bwawa hilo maalum.
"KUWASA, anzeni mchakato wa kutafuta eneo litakalojengwa bawawa maalum ambalo litakuwa ni mbadala wa chanzo cha maji cha ziwa Victoria ili liweze kusaidia pindi kunapotokea changamoto yoyote ikwenye chanzo hiki cha maji", amesema Mhe. Aweso.
Aidha Mhe. Aweso amesema Wizara ipo tayari kushirikiana na KUWASA ili kujenga bwawa hilo na kuondoa tatizo la maji kwenye Wilaya ya kahama inayojitokeza hasa tatizo la kiufundi linapojitokeza na kusababisha adha kubwa kwa wananchi wa Kahama.
Kufanikisha kwa upanuzi huu wa mtandao wa maji katika kata hii ya Isagehe uliogharimu zaidi ya Mil. 940 kunatajwa kuwa mwarobaini wa tatizo la maji lililodumu kwa muda mrefu eneo hili.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa