Na. Shinyanga RS
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 8 Desemba 2023.
Katika ziara hii Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Kahama Manispaaa.
Miundombinu hii iliyoharibiwa na mvua ni pamoja na barabara ya Shinyanga - Old Shinyanga, barabara ya Old Shinyanga - Solwa, barabara ya Solwa - Kahama na miundombinu mingine ya barabara.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa