Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya siku moja leo tarehe 10 Juni, 2019 katika Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini REA pamoja na kufuatilia uimara, matumizi na utunzaji wa nishati ya umeme.
Akizungumza na Viongozi na Watendaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara hiyo, Dkt. Kalemani amesema pia atatoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga miundombinu ya umeme wa REA awamu ya 3 ambaye hajaridhishwa na utendaji wake.
" Wananchi watulie kwani muda wa kumaliza kazi wa Mkandarasi kumalizia kazi bado unaendelea, Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 36 kwa Mkoa wa Shinyanga, lazima zitumike kuleta tija" amesema Kalemani.
Kalemani amesema lengo la Serikali ni vijiji vyote vipate umeme hivyo Shirika la Umeme Tanesco pamoja na REA wanashirikiana kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa